Kiazeri-Kaskazini
Mandhari
(Elekezwa kutoka Kiazeri ya Kaskazini)
Kiazeri-Kaskazini ni lugha ya Kiturki nchini Azerbaijan, Urusi, Georgia na Armenia inayozungumzwa na Waazeri. Ni lugha rasmi nchini Azerbaijan.
Ni lugha tofauti na Kiazeri-Kusini nchini Uajemi. Hata hivyo wengine huangalia hizo lugha mbili kuwa lugha moja tu, yaani Kiazeri.
Mwaka wa 2010 idadi ya wasemaji wa Kiazeri-Kaskazini nchini Azerbaijan imehesabiwa kuwa watu milioni nane na robo. Pia kuna wasemaji 473,000 nchini Urusi (2010), 360,000 nchini Georgia (2007) na 161,000 nchini Armenia (1993).
Kufuatana na uainishaji wa lugha wa ndani zaidi, Kiazeri-Kaskazini iko katika kundi la Kiturki cha Kusini.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- lugha ya Kiazeri za Kaskazini kwenye Multitree
- makala za OLAC kuhusu Kiazeri za Kaskazini
- lugha ya Kiazeri za Kaskazini katika Glottolog
- lugha ya Kiazeri za Kaskazini kwenye Ethnologue
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiazeri-Kaskazini kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |